MWANAMKE mmoja ambaye inasemekana alikuwa mgonjwa nchini Marekani ametoa kituko cha kufungia mwaka baada ya kuomba kucheza nyimbo ya mwanamuziki wa nchi hiyo Beyonce 'Get Me Bodied' katika chumba cha upasuaji.
Mwanamke huyo ametoa kituko hicho cha mwaka katika hospitali ya Mtakatifu Zion huko San Francisco nchini Marekani mwanzoni mwa mwezi huu ambapo alikuwa kwenye ratiba ya kufanyiwa upasuaji ingawa haikujulikana alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani.
Mgonjwa huyo ambaye alitambulika kwa jina la Deborah Cohan hakuonesha hali yoyote ya wasiwasi kuingia katika chumba hicho cha upasuaji kama walivyo wagonjwa wengine , na matokeo yake kuomba kucheza wimbo huo ambapo aliwashawishi madaktari waliokuwemo katika chumba hicho kuungana naye kucheza.
Ombi hilo lilikubaliwa na madaktari wote waliokuwemo katika chumba hicho ambapo walicheza kwa furaha kama wapo katika sherehe ya kupongezana.
Baada ya muimbaji Beyonce kuiona video hiyo ambayo inamuonesha mgonjwa huyo kucheza nyimbo yake kabla ya kuanza kufanyiwa upasuaji aliamua kumpa hongera ya ujasiri mwana mama huyo katika ukurasa wa Facebook.
Pamoja na hayo mwanamama huyo aliweza kufanikiwa kumaliza upasuaji wake huo salama huku akiendelea kupona taratibi taratibu kidonda chake hicho kwa mujibu wa taaliza zilizoandikwa kwenye mtandao wa Aceshowbiz Cohan.