Google PlusRSS FeedEmail

MILEY CYRUS AMUENZI 2PAC, NOTORIOUS


Msanii wa muziki nchini Marekani Miley Cyrus ameamua kuwaenzi wasanii wa muziki wa miondoko ya Hip Hop hayati 2 Pac na Notorious B.I.G kwa kuvaa gauni fupi lenye picha za wasanii hao.

Miley ameonekana akiwa na kivazi mwishoni mwa wiki katika hafla ya tuzo za MTV 2013 ambapo alivalia gauni hilo lenye sura za wasani hao kwa lengo la kuwaenzi marapa hao ambao walikuwa maarufu duniani.

Mbali na hayo pia star huyo alifanya  show katika hafla hiyo huku akipokea tuzo ya video bora kupitia wimbo wake unaojulikana kwa jina la 'Wrecking Ball'.

Muimbaji huyo aliwashangaza mashabiki wake ambapo alionekana akivuta kitu ambacho kilitambulika kuwa ni marijuani huku akitoa shukrani zake kwa watu waliomuwezesha kushinda tuzo hiyo jukwanii hapo.

Kilichowashangaza mashabiki wake hao ni kitendo cha muimbaji huyo kupanda jukwaani huku akiwa anavuta marijuana, ingawa alikuwa yupo katika mji wa Amsterdam ambapo ni ruhusa kuvuta hadharani na ndio maana aliweza kufanya hivyo bila ya kuchukuliwa hatua yoyote

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging