Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO, MADEE 'WALA BATA PAMOJA'


ILIDAIWA kuwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini wenye majina makubwa Ney wa Mitego, na Madee walikuwa kwenye ugomvi mkubwa huku ugomvi huo kila siku ukizidi kuchukua sura mpya kutokana na uchochezi uliokuwa unadaiwa kuchochewa na mitandao ya kijamii.

Katika hali ambayo si ya kawaida inadaiwa kuwa ugomvi huo unatokana na chanzo cha ubabe wa kila mmoja ndio anayeibeba Manzese na kuitangaza kwenye kazi za muziki wao wanaoufanya huku kila mmoja kwa wakati wake akijitapa kuwa yeye ndiye rais wa Manzese.

Lakini hali ambayo ipo kwa wasanii hao hivi sasa inaonekana ule ugomvi uliokuwa unasemekana upo umekwisha na sasa wanaonekana kuwa wapo karibu kila siku, huku wakiwa wanaonekana sehemu mbalimbali za kula bata pamoja na kufanya shoo jukwaa moja.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging