Mwigizaji wa kike wa filamu Wema Sepetu hivi karibuni alimpoteza baba yake mzazi aliyefariki katika Hospitali ya TMJ kufuatia msiba huo Wema alifunguka kwa kudai kuwa baba yake alikuwa kiungo muhimu sana katika harakati zake za urembo na sanaa kwa ujumla kwani baba yake alimuunga mkono katika kufanikisha ndoto zake.
“Nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu baba alikuwa akinisupport katika sanaa kwani hata awali nilipotaka kuingia katika mambo ya ulimbwende baba yangu aliniunga mkono, kulingana na nafasi yake kwa mzazi mwingine isingekuwa rahisi kunikubalia kuingia katika mashindano ya umiss,”anasema Wema.
Wema anasema hadi dakika za mwisho kabla ya baba yake kufariki alikuwa akimwita Miss world, hata alipoingia katika sanaa ya uigizaji wa filamu bado mzazi wake huyo alimuunga mkono jambo ambalo kwake lilikuwa ni faraja na kujivua kuwa na mzazi anayetambua umuhimu wa kipaji cha mwanaye.