Google PlusRSS FeedEmail

ANGEL KARASHANI AACHIA WIMBO MPYA



MUAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu mwaka huu ambaye alitolewa mapema katika kinyanganyiro hicho Angel Karashani, ametoa wito kwa watanzania kuwa na utaratibu wa kuwapigia kura kwa wingi vijana hao wa kitanzania pindi wapatapo nafasi ya kuwakilisha nchi.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Angel alidai kuwa kinachowafanya kutolewa kwa haraka katika mashindano hayo, kunatokana na kura zao kuwa chache tofauti na washiriki wengine ambao wanapigiwa kura na wananchi wao.

Alieleza kuwa hadi mwakilishi anapofika katika shindano hilo na kuingia katika hatua ya kuingia katika academia hivyo inaonesha anauwezo wa kuimba na kulimiliki jukwaa, kutokana na hatua hiyo ushindi unabaki mikononi mwa watanzania kupiga kura kwa wingi ili aweze kufanikiwa.

"Mimi nilitolewa kwa sababu kura zangu zilikuwa hazitoshi na siyo kwa sababu nilishindwa kuimba vyema au kulimiliki jukwaa hivyo watanzania wanatakiwa kushirikiana na washiriki kwa kuwapigia kura ili kuwawezesha kushinda" alisema Angel.

Pamoja na hilo msanii huyo ambaye nyota yake ilianza kung'ara aliposhirikishwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz katika wimbo unaojulikana kwa jina la Baadae, ambapo hivi sasa ametoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nisamehe.

Aliongezea kuwa anamini atafanya vyema katika soko la muziki kwa sababu anania ya kufanya hivyo, huku akizingatia ubunifu na kujitofautisha na wasanii wengine ili aweze kuwa msanii wa kimataifa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging