IRAKOZE HOPE AIBUKA KIDEDEA TPF
MWAKILISHI kutoka Uganda Irakoze Hope mwisho wa wiki hii ameibuka mshindi katika mashindano ya Tusker Project Fame,na kujinyakulia sh. Milioni 5 za Kenya ambazo ni sawa na milioni 90 za kitanzania.
Fainali hizo zilifanyika nchini Kenya ambapo mbali na kujishindia hela hizo pia mshindi huyo ameweza kupata mkataba wa mwaka mmoja wa kurekodi chini ya usimamizi wa Sony Music Afrika ambao mkataba huo unathamani ya sh. milioni 200 za kitanzania.
Katika mashindano hayo mwakilishi kutoka Tanzania anayejulikana kwa jina la Hisia aliweza kuonekana akifanya vizuri hadi kuingia katika hatua ya tano bora.
Ambapo katika kinyanga'nyiro hicho nafasi ya pili iliweza kukamatwa na Amos, Josh kutoka Kenya, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Daisy kutoka Uganda na nafasi ya nne ilichukuliwa na Hisia mwakilishi wa Tanzania.
Baada ya ushindi huo, Hope aliweza kuwashukuru mashabiki wake wote waliomuwezesha kushinda mashindano hayo kwa kumpigia kura kwa wingi.
Mbali na hayo washiriki wote waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora walipanda jukwaani kwa kuanza kutumbuiza nyimbo zao walizorekodi wenyewe pamoja na video zao walizorekodi.








