Google PlusRSS FeedEmail

HISIA AREJEA DAR, AVISHUKURU VYOMBO VYA HABARI



MWAKILISHI aliyewakilisha nchi katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa 6, Elisha Maghiya 'Hisia' amevishukuru vyombo vya habari, wadau wa muziki pamoja na wadhamini wa mashindano hayo kwa kumuwezesha kufika kwenye fainali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kurejea kutoka katika shindano hilo ambalo lilikuwa limefanyika nchini Kenya, alisema kuwa kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker kimemuwezesha kufika katika shindano hilo pamoja na kuwaamasisha wananchi kumpigia kura.

Alisema kuwa vyombo vya habari vimefanya kazi kubwa pia ya kuhamasisha watu pamoja na kuwaelimisha juu ya mashindano hayo hali ambayo imeibua hisia zao na kusababisha kumpigia kura kwa wingi.

Alisema kuwa alikuwa na uwezo wa kushinda shindano hilo, endapo kura zake zingetosha, ila ameshindwa kuchukua nafasi hiyo kutokana na kura zake kutofikia kiwango cha kumuwezesha kuwa mshindi.

Alisema kwa hatua aliyofikia, ameweza kuitangaza vyema nchi ya Tanzania na kuibua ushindani mkali ndani ya academia hiyo kutokana na uwezo aliokuwa nao wa muziki.

"Kiukweli kufika hatua niliyofika ni kwa sababu ya wananchi kunipigia kura kwa wingi ' team hisia ', wameniwezesha nifike hapa nilipo hizi ni kwa nguvu zao, ingawa bado wanatakiwa mashabiki kuendelea kuelimishwa juu ya umuhimu wa kupiga kura" alisema Hisia.

Aliongezea kuwa kura ndizo zinazomchagua mshindi, hivyo mshindi alijulikana katika shoo ya mwisho ambayo ilifanyika siku ya Jumamosi, hali ambayo shoo ya fainali haiwezi kubadili matokeo hayo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging