Msanii kutoka nchini Canada Justin Bieber, awatembelea waathirika wa kimbunga pamoja na kutoa misaada kwa watu hao ambapo kimbunga hicho kilitokea hivi karibuni nchini Ufilipino.
Kwa mujibu wa Associated Press, alidai kuwa ziara ya Bieber nchini Ufilipino ni moja ya jitihada za nyota huyo kutoka Canada kwa ajili ya kutoa misaada kwa wale waliopatwa na janga la kimbunga nchini humo.








