Google PlusRSS FeedEmail

HISIA KUJA NA 'MAWAZO'



MUIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini Elisha Simon 'Hisia' hivi karibuni anatarajia kuachia  nyimbo yake mpya itakayojulikana kwa jina la 'Mawazo' , ambayo imebeba ukweli wa jambo lililowahi kumtokea katika maisha yake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa nchini Nairobi, Hisia aliweka wazi kuwa hivi sasa yupo katika maandalizi ya mwisho ya kutengeneza nyimbo hiyo ambayo ameitengeneza katika mtindo tofauti na uliozoeleka.

Nyimbo hiyo ambayo itakamilisha nyimbo mbili tangu amalize mashindano ya Tusker Project Fame, Hisia aliweka wazi kuwa nyimbo hiyo imetengenezwa tofauti  na anaamini itafanya vizuri.

Alisema kuwa nyimbo hiyo imefanywa 'live' ambapo vyombo vyote vya muziki vitasikika hali hiyo itasababisha nyimbo hiyo kuonekana yenye utofauti na mvuto  wa kipekee.

Akielezea alichokiimba kwenye nyimbo hiyo Hisia alidai kuwa nyimbo hiyo ni ya historia ya kweli ambayo teyari ilishawahi kumtokea kwenye maisha yake, ingawa imemtokea mara baada ya kumaliza kuiandika nyimbo hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging