Google PlusRSS FeedEmail

PROFESSA JAY KUUNGANA NA DIAMOND PLATNUM



MSANII wa miondoko ya Hip Hop nchini Joseph Haule 'Professa Jay'  yupo katika hatua za mwisho kurekodi nyimbo yake mpya ambayo amemshirikisha  msanii nyota wa muziki wa bongo fleva nchini Diamond Platnum.

Nyimbo hiyo ambayo bado hajafahamika jina lake inatengenezwa katika studio ya Bongo Records chini ya mtayarishaji mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini P -Funk Majani.

Inadaiwa kuwa wimbo huo utakuwa wa kihistoria kwa kuwa ni moja ya kazi inayomkutanisha tena Professa Jay pamoja na mtayarishaji huyo baada ya miaka mingi kutofanya kazi pamoja.

Mtayarishaji huyo ndiye pekee aliyeweza kumtengenezea nyimbo msanii huyo wa Hip Hop mika kadhaa nyuma zilizofanya vyema katika soko la muziki huku baadhi ya albamu kuwa ni albamu bora ya mwaka .

Professa Jay alituma picha kwenye ukurasa wake wa Istagram unaomuonesha akiwa studio ambapo ameambatana na msanii mkali huyo wa bongo fleva Diamond.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging