BARACK OBAMA KUHUDHURIA HARUSI YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN
May 24, itakuwa ni siku ya pekee katika maisha ya Kanye West na Kim Kardashian ambao wanatarajia kufunga ndoa siku hiyo.
Kumekuwepo na taarifa kuwa kutakuwa na upekuzi na ulinzi wa hali ya juu katika tukio hilo litakalofanyika Paris, Ufaransa huku wageni waalikwa wakizuiwa kuingia na simu isipokuwa Jay Z na Beyonce.
Kwa mujibu wa jarida la American Heat, tayari Kanye West amewapa wasaidizi wake orodha ya wageni 600 watakaohudhuria ndoa hiyo na kwamba katika majina hayo yumo mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Mandela, mrembo wa Kenya Lupita Nyong’o na malkia wa talk show Oprah Winfrey.
Orodha hiyo imeonekana kuwa na majina mengi ambayo huenda hawakutegemea, lakini kubwa zaidi ni mualiko alioupeleka ikulu ya Marekani kwa familia ya rais Barack Obama.
Mbali na majina hayo wamo Beyonce, Jay Z na Jimmie Foxx, Prince.








