Rapper The Game anakabiliwa na kesi ya kumshambulia kwa kipigo kikali mpenzi wake wa zamani, Tiffney Cambridge. Ambapo kwa mujibu wa ripoti za polisu, Tiffeney ambaye alizaa watoto wawili na The Game alifungua mashtaka dhidi ya The Game wiki iliyopita kufuatia ugomvi uliozuka kati yao March 19 mwaka huu.
Chanzo cha karibu na Tiffney kimeiambia Nicolebitchie kuwa rapper huyo alimpiga ngumi kadhaa usoni na kumuumiza jicho na pua. Lakini pia chanzo kingine kimeeleza kuwa polisi wana picha za uso wa Tiffney baada ya kipigo hicho.
Ripoti zimeeleza kuwa polisi wa Los Angeles tayari wameanza kufanya upelelezi kuhusu tukio hilo.
Ingawa The Game hakuongea sana kuhusu tukio hilo, alionesha kuwepo na dalili za ugomvi kati yao na kwamba hakuwa kumpiga mrembo huyo.
Lakini mwishoni mwa wiki hii alipost kwenye Twitter yenye maandishi haya:
“You are allowed to terminate toxic relationships. You are allowed to walk away from people who hurt you. You are allowed to be angry and selfish and unforgiving. You don’t owe anyone an explanation for taking care of yourself.”
The Game akikutwa na hatia anaweza kukutwa na msala ulimkuta Chris Brown mwaka 2009 baada ya kumpiga vibaya Rihanna, msala unaomsumbua hadi leo.








