Google PlusRSS FeedEmail

B'HITZ YAJIPANGA KUJA NA UJIO MPYABAADA ya ukimya wa muda, Studio za B’Hitz zimetangaza ujio wao mpya na kundi jipya ambalo watafanya nalo kazi rasmi, kundi lililobatizwa jina la ‘DISTRICT 9’.

B’Hitz inatangaza ujio wa kundi jipya ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuwaondoa kwenye label yake wasanii kadhaa waliokuwepo. CEO na Producer wa B’Hitz, Hermy B ametangaza ujio wa kundi hilo huo kupitia akaunti yake ya Instagram na kuweka kionjo/Snippet cha wimbo wa kwanza wa kundi hilo.

“B’hitz is back....Introducing DISTRICT 9...this is just a snippet of whats about to come out very soon...ya'll get ready...#DISTRICT 9” Ameandika Hemy B.

Ujio wa kundi hilo ambalo wasanii wake hakuwataja jina, unaonekana umeiva tayari kwa kuwa mbali na kuweka kionjo cha wimbo wao, ameonekana akichat na mtayarishaji wa video aliyeongoza video ya wimbo wa Lady Jay Dee ‘Historia’, Hefemi ambaye yuko nje ya nchi.

DISTRICT 9 itakuwa imeundwa na wasanii gani wa Bongo? Bado haijajulikana lakini kwa kuwa video ishatangazwa tutawaona…na ngoma mpya soon tutaisikia na kujua ‘District 9’.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging