Google PlusRSS FeedEmail

HALI YA MH VICKY KAMATA YAZIDI KUIMARIKA

                      

Staa wa Bongo Fleva na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha Vijana Mkoa wa Geita, Vicky Pascal Kamata akiwa na mchumba wake Charles Pai.
Ile harusi ya the Century iliyokuwa ifanyike jumamosi tar 24/05/2014 Kempisk Hotel baina ya Mbunge Maarufu wa Viti Maalum CCM Mh. Vicky Kamata imepiga mwamba kutokana na ukweli kujulikana dakika ya mwisho jana kwamba Mchumba wake Mheshimiwa Mbunge ni Tapeli wa ajabu hapa nchini amabae amekuwa akiwadanganya sana kina dada wenye utajiri na kwamba Mh. Vicky Kamata anakuwa ni Mbebez wa tatu kutapeliwa na Mchumba huyu pichani.


Ripoti inasema kwamba Juzi Mke wa kweli wa Mchumba huyo alijitokeza na hati zake Kanisani Catholic kwa Wachungaji waliomfahamisha Mchumba kwamba hakutakuwa na tendo la kufunga Ndoa Kanisani ndipo Mchumba huyo bwana Charles akatimka na jumla ya pesa za mchango wa harusi hiyo Shillingi Millioni 40. Jumla zilikuwa zimeshachangwa Shillingi Millioni 100, tayari USD $ 15,000 zilikuwa zimeshalipiwa kwa ajili ya Ukumbi wa Kempisk Hotel, tayari wageni waalikwa toka Geita walioshiriki kumchagua Mbunge huyo walishafika Dar wapo hapa, na cha kutisha zaidi ni kwamba Mheshimiwa Mbunge toka jana asubuhi ameshindwa kabisa kumpata mchumba huyo kwenye simu zake zote zimezimwa hazipatikani kabisa. Inasemekana baadhi ya Wabunge waliomchangia kwa kiwango kikubwa sana wameanza kulalamika kwa pembeni.                       

                       
This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging