Google PlusRSS FeedEmail

HATIMAYE FID Q ABEBA TUZO, DIAMOND AWEKA HISTORIA KTMA 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum akiwa ameshikiria tuzo huku Ommy Dimpoz akitoa neno la shukrani kwa niaba yake.

Tuzo za Muziki za Tanzania, zinazojulikana kwa jina la Kilimanjaro Music Awards (KTMA2014), hatimaye zimefikia tamati jana katika ukumbi wa Milimani City, Dar es Salaam ambapo Diamond Platinumz aling’aa zaidi na kuweka historia kwa kuondoka na tuzo saba, katika vipengele vyote saba.

Aliweza kuweka historia nzuri hiyo jana ambapo aliweza kuondoka na tuzo kwa kila kipengele alichoshindanishwa hali iliyosababisha kumfanya aweke historia katika muziki wake na kwa upande wa tuzo hizo.

Diamond alishinda tuzo ya Video bora ya mwaka (My Number One), Muimbaji bora wa kiume-Kizazi kipya, mtumbuizaji bora wa kiume –Kizazi kipya, Mtunzi bora wa mwaka – Kizazi Kipya, Wimbo bora wa Afro Pop, Wimbo bora wa mwaka na Wimbo bora wa kushirikiana alioshirikishwa na Nay wa Mitego (Muziki Gani).

Kwa upande mwingine Wema Sepetu alionekana kuwa kivuto zaidi ambapo aliweza kumpa mpenzi wake huyo kampani mara zote alizokuwa akiitwa kupanda jukwaani.

Kwa upande wa hip hop rapper wa Mwanza Fid Qaliweka historia ambapo kwa mara ya  kwanza alishinda tuzo mbili. ikiwa  tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop na mtunzi bora wa mwaka –hip hop.

Kundi la Weusi pia lilibeba tuzo mbili ambazo ni Kikundi cha Mwaka cha Kizazi Kipya na Wimbo bora wa mwaka (Nje ya Box- Nikki wa Pili feat. Joh Makini &G-Nako).

Rapper Young Killer pia alifanikiwa kuibeba tuzo kwa mara ya kwanza ambapo alishinda tuzo ya Msanii bora anayechipukia.

Kwa upande wa Bendi, mwanamuziki kutoka Congo, Christian Bella alikuwa sura mpya katika tuzo hizo mwaka huu na aliondoka na tuzo ya Mtunzi bora wa mwaka.

Tuzo hizo zilipambwa na burudani safi toka kwa wasanii mbambali walioonesha uwezo wa hali ya juu ya kutumbuiza; Mwana FA, Kundi la Weusi, Vanessa Mdee, Makomando, Madee, Ommy Dimpoz, Diamond, Meninah, Angel, bendi za Extra Bongo na Twanga Pepeta na wengine.


Angalia orodha kamili ya washindi KTMA2014:
Wimbo bora wa mwaka

Number One – Diamond

Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya

Lady Jaydee

Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya

Diamond

Muimbaji bora wa kike taarab

Isha Ramadhan

Muimbaji Bora wa kiume – Taarab

Mzee Yusuf

Muimbaji bora wa kiume – Bendi


Jose Mara

Muimbaji Bora wa Kike – bendi

Luiza Mbutu

Msanii Bora wa Hip Hop

Fid Q

Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia

Young Killer

Rapa Bora wa Mwaka – Bendi

Furguson

Mtumbuizaji bora wa kike muziki

Isha Ramadhani

Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki

Diamond

Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop

Fid Q

Video Bora ya Mwaka

Number One – Diamond

Bendi ya Mwaka

Mashujaa Band

Kikundi cha Mwaka cha Taarab

Jahazi Modern Taarab

Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya

Weusi

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab

Enrico

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Kizazi kipya

Man Walter

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Bendi

Amoroso

Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab

Mzee Yusuf

Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya

Diamond

Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi

Christian Bella

Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi

Ushamba Mzigo – Mashujaa Band

Wimbo bora wa reggae

Niwe na Wewe – Dabo

Wimbo bora wa Afrika Mashariki

Tubonge – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Afro Pop

Number One – Diamond

Wimbo bora wa Taarab

Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf

Wimbo bora wa Hip Hop

Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako

Wimbo Bora wa R&B

Closer – Vanessa Mdee

Wimbo Bora wa Kushirikiana

Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond

Wimbo bora wa ragga/dancehall

Nishai – Chibwa f/ Juru

Wimbo bora wa zouk /rhumba

Yahaya – Lady Jaydee

Hall of FAME Award

Hassan Rehani Bichuka

Masoud Masoud & TBC Taifa

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging