Google PlusRSS FeedEmail

HUDDAH ATOA YA MOYONIMitaa ya Kenya kuna habari zilizovujishwa na shushushu mmoja aliyeripoti kwa mtandao wa Ghafla akiambatanisha na picha kuwa mshiriki wa BBA ‘The Chase’ Huddah Monroe amefulia.

Kwa mujibu wa taarifa za mdaku huyo, mrembo huyo amefukuzwa kwenye nyumba ya kishua baada ya kushindwa kulipia kodi na hivyo amehamia maeneo ya Parklands na anaishi na mwanaume ambaye hafahamiki.

Picha hizo zinamuonesha Huddah akiwa amekumbatiwa na mwanaume huyo na nyingine wakiwa wamekaa na amemshika mabegani.

Hata hivyo sio kila ushahidi wa picha halisi ni wa kweli, mrembo huyo alipotafutwa alikanusha na kuzifanyia utani taarifa hizo na kudai kuwa yeye anaishi Kilimani na sio Parklands na kwamba mtu anaeonekana nae kwenye picha hiyo ni ndugu yake.

“He’s crazy! I live in Kilimani. That’s my cousin’s pal and that’s his house in Park Road.” Amesema Huddah Monroe.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging