VIDEO YA WIMBO WA KUNDI LA SAUTI SOL YAFUNGIWA KWA MADAI YA KUCHOCHEA NGONO
Posted on by Zourha Malisa
Video ya wimbo wa Nishike wa kundi la Sauti Sol la Kenya ambayo imeangaliwa zaidi ya mara 147,800 tangu itoke April 29, imefungiwa na vituo vya runinga vya Kenya baada ya kuona inakiuka maadili.
Kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla, member wa kundi hilo Bien Aime alieleza kuwa video hiyo imefungiwa na vituo vya runinga kwa madai kuwa inachochea ngono.