Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MASHABIKI, MASANJA AFUNGUKA ADAI HAONI UMUHIMU WA KUWEKA PICHA YA MAREHEMU KWENYE MITANDAO


MSANII wa vichekesho nchini Masanja, ameweka wazi kuwa hatoweka picha ya marehemu msanii yoyote yule kwenye mitandao ya kijamii, kwani haoni umuhimu wa kufanya hivyo zaidi ya kumshukuru mungu moyoni kwa lolote analotenda.
 
Aliandika hayo kupitia ukursa wake wa istagram mara baada  kwa siku mbili mfululizo baadhi ya mashabiki wa sanaa Tanzania waliwashambulia Diamond Platinumz na Masanja Mkandamizaji kwa kutoweka kitu chochote ikiwemo picha za misiba ya wasanii wenzao kwenye mitandao ya kijamii.
 
Hali hiyo iliibuka mara baada ya taalifa kuthibitishwa juu ya kifo cha muongozaji wa filamu pamoja na vipindi vya Televisheni nchini, George Tyson kilichotokea mkoani Morogoro kilichosababishwa kwa ajali ya gari, baadhi ya wasanii wajikuta kwenye hali ngumu kwa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki wao kwa kushindwa kutoa pole kwenye kurasa zao za mitandao kama ambavyo wasanii wengine wanavyofanya.
 

Wakati huo wawili hao walionekana wakituma picha wakiwa wapo sehemu mbalimbali za kula starehe 'kula bata' kama vile hakujatokea kitu chochote kwenye familia yao ya sanaa hali hiyo ilizusha maswali mbalimbali kwa mashabiki hao.
 
Ukurasa wa Diamond ulisomeka hivi “Asante Mungu North Carolina's Safe! #BadaeHudumaInaanzaa", huku wa Masanja nao ukisomeka  "JumapiliMapemaaIbadaYaKwanzaWashingtonDc" wakati huo kurasa za wasanii wenzao zilikuwa zikisomeka taarifa ya msiba pamoja na picha ya mtayarishaji huyo.
 
Hali hiyo ilizua utata kwa mashabiki wao kwani walijikuta wakishambuliwa na mashabiki wao huku wengine wakihoji juu ya taalifa hizo za misiba na hali ikoje, huku wengine wakiweka wazi kuwa walitarajia kuona wakiungana na wenzao kwa kupost picha na salamu za rambilambi.

Ambapo baada ya maoni na maneno ya kushambuliwa kupitia ukursa wa Istagram Masanja akaamua kuweka wazi juu ya uamuzi wa kutoweka picha yoyote ile ya msiba kwani hata kwa upande wake yeye alifiwa na hakuweka picha yoyote ile zaidi ya kuomboleza moyoni.
 
Hata hivyo, baada ya makombora ya mashabiki hao, Diamond Platinumz aliandika post kuhusu misiba ya wasanii walipoteza maisha katika kipindi kifupi, Adamu Kuambiana, Rachael Haule na muongozaji wa filamu George Tyson.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging