Google PlusRSS FeedEmail

PROFILE: MZEE SMALL


Said Ngamba au Mzee Small amezaliwa mwaka 1955 alikuwa msanii wa maigizo na vichekesho kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anaaminika zaidi kuwa ni mmoja wa wasanii wakongwe kwa nchi ya Tanzania, hasa katika fani ya uchekeshaji ambayo sasa inachezwa zaidi na vijana.

Mzee Small alizaliwa mwaka 1955 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, pia Mzee Small kila unapozungumza naye huwa na kawaida ya kujitamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha katika luninga.

Pamoja na kuwa yeye ndiyo mwanzilishi wa kuonyesha vichekesho kupitia luninga, lakini bado amesimama kufanya maigizo ingawaje alianza sanaa hiyo miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na Bw.Said Seif ‘Unono’ (ambaye kwa sasa ni marehemu).

Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, pia Mzee Small amecheza sanaa katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo unaojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule unaomwelezea mwanamke mmoja wa kijijini aliyeolewa mjini.

Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small pia ni mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye Haki.

Pia aliwahi kuibuka na kitu kingine kiitwacho “Nani Kama Shule" huku akiwa amewashirikisha wakina Majuto, Kingwendu nawachekeshaji wengine wanaotamba sasa nchini Tanzania.

Mzee Small alishawahi kumiliki kundi lake la sanaa linalojulikana kama Afro Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 BASATA, na kupata usajili rasmi mwaka huohuo wa 1994.

Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini hakuwa na mpango wowote ule wa kujiunga na kundi jingine, ila anachoweza kufanya ni kurekodi na wasanii wengine atakapoitwa kwa makubaliano maalum. Mzee Small aliwahi kuzungumza hilo kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya kabla ya kufikwa na umauti.

Kutokana na vichekesho, Mzee Small huwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua kinachoendelea kuwa ni kazi tu. Mzee Small ameacha watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike

HALI YA UGONJWA

Wakati akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka jana’ Mzee Small aliripotiwa kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye shughuli za kisanaa Kanda Ziwa.Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za usiku Juni 7, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging