Google PlusRSS FeedEmail

SAUTI YA KAMANDA WA POLISI AKIELEZEA TUKIO LA KANGA MOKO KUPIGWA RISASI


JESHI la polisi limeanza kufanya uchunguzi tukio la watu wawili wakazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam, wanaodaiwa kujeruhiwa katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na Askari Polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma za wanenguaji maarufu 'Kanga moko', ambazo tayari zimepigwa marufuku na Jeshi la Polisi nchini.

KAMANDA wa Polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, la wadada hao wawili pamoja na mkaka mmoja wanaodaiwa kupigwa risasi ingawa bado haijathibitishwa.

Wambura aliendelea kuweka wazi kuwa hakukuwa na uthibitisho wowote wa watu hao kupigwa risasi ambapo jeshi la polisi linafanya uchunguzi wake wa kina ili kubaini kama tukio hilo limetokea kwa kupigwa risasi, kumbaini ni nani aliyepiga risasi hiyo.

Kamanda huyo alidai kuwa uchunguzi wa awali ulibainisha kuwa kulitokea na vurugu wakizuiliwa kutocheza uchi katika ngoma hiyo maarufu jijini Dar es Salaam ya wanenguaji hao maarufu 'Kanga moko', ambayo ipo kinyume cha maadili.

Aidha, taarifa zimesema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18, 2014 saa kumi na nusu jioni katika eneo la Shule ya Msingi Kisiwani ambapo tovuti hii imejulishwa kuwa kati ya majeruhi wawili mmoja tayari yao ameruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala jijini humo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging