Google PlusRSS FeedEmail

JUSTIN BIEBER NA PICHA ZA MPENZI MPYA


MMOJA wa wapiga picha amezibamba picha zinazomuonesha muimbaji kutoka Marekani Justin Bieber akiwa anajivinjari na msichana huku wakiwa kwenye pozi linaloashiria wawili hao ni wapenzi.

Bieber alionekana akiwa na mwanamke huyo asiyejulikana ambapo msanii huyo alitumia muda wake kwenda kupumzika kwenye visiwa vya Ibiza.

Pop star Justin Bieber aliungana na Kanye West,Kim Kardashian,P.Diddy na mastaa wengine kwenye mapumziko kwenye visiwa vya Ibiza. Baada ya party ya pamoja kuisha kila mtu aliendelea na party kivyake na Justin Bieber alionekana aki-enjoy muda wake na msichana asiyejulikana.

Mikao yao na ukaribu wao kutokana na picha zilizopigwa wakiwa kwenye luxury yacht zinaonyesha kabisa wapo kwenye mapenzi. Wawili hao walitumia muda huo kukaa pamoja,kissing,kunywa na vitu vingine vizuri. Mapaparazi hawakuwaacha baada ya kuwapiga picha usiku huo kwasababu hadi asubui walipata picha zao bado wapo pamoja.

Tetesi zinasema kwamba anaweza kuwa ni girlfriend mpya wa Justin Bieber.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging