Google PlusRSS FeedEmail

JAY AIELEZEA TATU CHAFU


MSANII wa muziki wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop Joseph Haule ‘Professor Jay’ amewataka wasanii chipukizi wanaibukia kwenye gemu la muziki kuendelea kuwaheshimu wasanii wakongwe waliowafungulia njia.

Ambapo inadaiwa wapo baadhi ya wasanii chipukizi wanaoibukia kwenye gemu la muziki wanashindwa kuwaheshimu wasanii wakongwe ambao wao ndio waliowafungulia njia katika muziki nchini na kuutambulisha muziki huo ambao hao awali ulionekana kama ni muziki wa kihuni.

Akizungumza na jarida hili, wakati akieezea alichokifikiria kuimba katika nyimbo yake mpya ya Tatu Chafu, msanii huyo alieleza kuwa kabla ya kuimba wimbo huo alifikiria jinsi baadhi ya wasanii wanaochipukiz kudharau wasanii wakongwe.

Alisema kuwa kwenye nyimbo hiyo ya Tatu chafu, aliitengeneza mahususi kwa ajili ya kuwakumbusha mashabiki wake ambao walimsahau Yule Profesa jay wa kipindi hicho ambaye alikuwa akianza muziki akitembea na makalatasi mengi mfukoni kuliko hela.

“Unajua nilipoanza muziki kipindi hicho nilikuwa natembea na makaratasi mengi mfukoni kuliko hela yaani nilikuwa nauhangaikia muziki wangu ambao hivi sasa umenifikisha hapo, sitembei tena na makaratasi bali natembea na mkwanja” alisema Jay.

Ambapo aliongezea kuwa nyimbo hiyo amewashirikisha watu wawili ambao wote ni yeye huku akifafanua zaidi yeye alianza muziki akiwa anaimba kingereza, na baadae akaanza kufoka na sasa anaimba muziki huu kwa mtindo huu wa mashabiki wanaomsikia.



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging