Google PlusRSS FeedEmail

WASANII ACHENI UOGA SAMBAZENI KAZI ZENU- MTITU

                    William j. mtitu
Mtayarishaji na muongozaji wa filamu Bongo William J. Mtitu ‘Mtitu’ amewashauri wasanii na watayarishaji wenzake wa filamu kuacha kuwategemea wasambazaji wanaowanyonya na kuwasumbua badala yake waache woga na kuingia kusambaza kazi zao kama alivyofanya yeye.

“Kama unaishi hauwezi kukwepa changamoto unazokutanazo, lazima upambane nazo nawashauri wasanii wenzangu kuachana na kuwategemea wasambazaji bali wasambaze wenyewe kazi zao, ni uamuzi tu,”anasema Mtitu.

Mtitu ambaye namiliki kampuni ya 5 Effect inayotengeneza filamu na kusambaza amefanikiwa kwa kuweza kusambaza kazi zake bila kutegemea wasambazaji wengine, anasema ukisambaza mwenyewe hauuzi haki ya filamu yako.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging