Google PlusRSS FeedEmail

MARIAH CAREY ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 41 KUWABURUDISHA MBWA WAKE

Utafanya nini ukipewa kiasi cha Milioni 41 za kitanzania muda huu? Bila shaka utapanga mengi na wazo kubwa likiwa kuuaga umasikini kwa muda kama hukuwahi kuzishika.

Lakini Mariah Carey ametumia kiasi hiki cha fedha kuwaburudisha mbwa wake kwa kuwapangishia chumba katika hotel ya kifahari, Bristol.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Mariah amelipia kiasi cha zaidi ya $25,000 (zaidi ya Milioni 41) ili mbwa wake hao wapewe huduma daraja la kwanza katika hotel hiyo ya kifahari.

Mbwa hao wamepewa chumba chao pekee, wanahudumiwa chakula kizuri kinachopikwa na mpishi wao maalum katika hotel hiyo, watapelekwa kuogelea na kutembezwa katika maeneo mazuri ya hotel, wataangalia games na movies ambazo zinahusu mbwa.

Katika hatua nyingine, Mariah Carey ameripotiwa kusitisha kufanya kazi na Jermaine Dupri aliyekuwa meneja wake na mshikaji wake kwa kipindi kirefu. Hatua hii inakuja wakati ambapo albam yake mpya ‘Me. I am Maria…’ ambayo tangu itoke May 23, mwaka huu imeuza nakala 103,000 tu.

JD amethibitisha uamuzi wa Mariah Carey na kueleza kuwa wataendelea kufanya kazi siku za usoni. Inaelezwa kuwa Mariaha amenza kufanya kazi chini ya Kevin Liles aliyewahi kuwa rais wa Def Jams.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging