Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA MAPYA YAIBUKA KWA MTOTO WA JACKIE CHAN

Mtoto wa Jackie Chan ambaye pia ni muigizaji wa filamu za mapigano, Jaycee Chan anaendelea kushikiliwa na polisi nchini China kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa polisi wa Beijing, Jaycee alikamatwa akiwa na muigizaji mwenzake wa Taiwan, Kai Ko na kwamba baada ya kupimwa waligundulika kuwa walikuwa wametumia dawa za kulevya aina ya marijuana.

Jaycee na Kai Ko wamekiri kutumia dawa hizo na kueleza kuwa grams 100 za dawa hizo zilipelekwa nyumbani kwa Jaycee (mtoto wa Jackie Chan).

Baada ya kushikiliwa kwa wiki mbili (tangu August 14), Kai Ko ameachiwa Ijumaa iliyopita na anasubiri taratibu zaidi za kisheria huku Jaycee akiendelea kusota rumande.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Beijing, waandishi wa habari walimfuata Kai Ko hadi kwenye hotel aliyofikia lakini hakuonesha ushirikiano na alijaribu kumpiga mwandishi mmoja kabla hajaingia kwenye lift na kutokomea.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo, Jackie Chan aliomba radhi umma kwa niaba ya mwanae na familia yao kwa ujumla alimtaka mwanae kuelewa kuwa amefanya makosa na anapaswa kukutana na matokeo yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging