Google PlusRSS FeedEmail

JENNIFER ALAANI KITENDO CHA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUWEKWA MITANDAONIMsemaji wa muigizaji wa kike Jennifer Lawrence amelaani kitendo cha watu kupost picha za utupu za Jennifer Lawrence zilizovujishwa na hackers walioziiba kwenye simu yake.

Msemaji huyo ameeleza kuwa tayari wameongea na vyombo vya usalama na watamfungulia mashtaka mtu yeyote atakayepost picha hizo zilizoibiwa.

Jumapili iliyopita kuna post nyingi za Twitter, Tumblr, Reddit na nyingine ambazo zinaelezwa kuwa na picha hizo za utupu za Lawrence ambaye ni mshindi wa tuzo za Oscar pamoja na msataa wengine.

Kwa mujibu wa Mirror, hackers wameeleza kuwa wana video nzima ya Jennifer akiwa mtupu na picha chafu zaidi ya 60 na wamepanga kuendelea kuzitoa.

Kwa upande wa wamiliki wa mtandao wa Twitter, wameichukulia hatua hiyo kama uvunjifu wa haki ya kuwa na faragha (privacy) na wamezifuta akaunti zote zilizopost picha hizo.

Imeelezwa kuwa hackers wamepata picha za utupu kutoka kwenye simu za watu maarufu zaidi ya 100 na wamepanga kuzisambaza.

Hata hivyo mwakilishi wa Arianda Grande ambaye picha zake zilisambaa pia Jumapili, ameeleza kuwa picha hizo zilizomuonesha akiwa mtupu hazikuwa halisi.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging