“Tunaomba juhudi hizi za ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili, muwasaidie wasanii wa filamu na muziki katika utunzi wao, watumie Lugha fasaha kwani wao ni rahisi kuwafikia watu kwa kutumia Filamu,”alisema Balozi Dkt. Burian.
Chawakama wamepongezwa kwa juhudi zao za kukuza Kiswahili Afrika ya Mashariki na nje ya Jumuia hiyo, Balozi Dkt. Batilda amesema Tanzania ina mpango kufungua vituo vya kufundishia Kiswahili katika nchi za Afrika ya Kusini, Rwanda, Burundi, Nambia na nchi nyingine.
Zaidi ya watu milioni 90 inasemekana hujifundisha Lugha ya Kiswahili kwa kutumia filamu za Kitanzania ikiwa kama ni njia rahisi kwao kujifunza Kiswahili, nchi nyingi za Scandinavia hutumia njia hiyo, ni fursa nyingine kwa watengenezaji wa filamu Swahilihood kuitumia.