Google PlusRSS FeedEmail

ROBIN THICKE AKIRI KUWA TEJA

Mwimbaji Robin Thicke ambaye yuko kwenye wakati mgumu hivi sasa baada ya kuachwa na mkewe, maji ya shingo yamemfika na ameamua kuweka ukweli hadharani kuufuta uongo mkubwa alioutengeneza kuhusu wimbo wa Blurred Lines.

Katika document aliyopeleka mahakamani na kunaswa na Hollywood Reporter katika kesi inayomkabili ya wizi wa mashairi ya wimbo wa Mavin Gaye wa mwaka 1977 ‘Got to Give Up’ iliyofunguliwa na watoto wa mwimbaji huyo ambaye ni marehemu wakidai ametumia bila kibali mashairi ya wimbo wa baba yao kwenye wimbo wake wa Blurred Lines, Robi

Thicke ameeleza kuwa yeye hakuhusika katika uandishi wa wimbo huo kama alivyodai awali na kwamba wimbo wote umeandikwa na Pharrell Williams.

Ameeleza kuwa alilazimika kusema uongo kwenye media kuwa alihusika kwa kuwa wimbo uligeuka kuwa mkubwa na yeye aliona wivu na alitaka apate ‘credit’ za kuhusika lakini ukweli ni kwamba wakati wimbo unaandikwa alikuwa hoi kwa ulevi japo alikuwa studio.

“Nilipata wivu na nilitaka nipate credit..nilijaribu kupata credit baadae kwa sababu Pharrell aliandika kitu chote mwenyewe na nilikuwa natamani hicho.” Ameeleza kwenye maelezo hayo.

Ameongeza kuwa ingawa Pharrell Williams ndiye aliyetayarisha mdundo na kuandika wimbo wote wakati yeye akiwa hoi hapo studio kwa Vicodin na pombe, Pharrell alimpa haki katika wimbo huo hadi zile ambazo hakustahili na ulipokuwa mkubwa na kumpa mafanikio makubwa duniani. 

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging