Google PlusRSS FeedEmail

TUNAPIGANIA MASLAI KWA AJILI YA WOTE

Simon Mwakifwamba, Samwel sitta
RAIS wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amefunguka kuwa shirikisho lao linajishughulisha na maslahi ya wasanii wote wa filamu na si kutumia muda mwingi kwa ajili ya matamasha na misiba hiyo si kazi yao.

       simon mwakifwamba, mizengo pinda john kitime

“TAFF inadili issue muhimu hatuhangaiki na mbwembwe za kujinuisha na misiba au matamasha, tunaangalia mustakabali wa Sanaa yetu, na tumefanya lobbying kwa waheshimiwa Wabunge kwa mara ya kwanza tasnia ya filamu na muziki itaongelewa katika katiba,”anasema Mwakifwamba.

Rais huyo amedai kuwa shirikisho lao limekuwa mbele kupigania maslahi ya wasanii wote pasipo ubinafsi wa kujitengenezea fedha kwa kutumia wasanii na wanaonufaika ni wachache na kuichafua tasnia nzima na kuonekana haifai ikiongoza kwa kashfa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging