Google PlusRSS FeedEmail

MOHAMED MWIKONGI AULIZA RIYAMA NIMEKUKOSEA NINI?

         Mohamed MwikongiMOHAMED Mwikongi ‘Frank’ muongozaji na na mwigizaji nyota amefunguka kwa kuelezea fitina na ubaya ambao amekuwa akifanyiwa Bongo Movie umemtisha na anahisi sasa anatafutwa roho yake, kwani mara nyingi anapigwa vita hadharani kutoka kwa wasanii wenzake ambao ujifanya ni marafiki.

Frank anaelezea hayo baada ya mtayarishaji wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni kuweka bayana kuwa yeye hakumhitaji Issa Mussa katika filamu yake bali aliyemchagua alikuwa ni Frank na baadae Riyama akamlaghai kwa kumueleza kuwa Frank ni msumbufu bora ampe nafasi hiyo Cloud.

“Naomba watu waniulizie dada yangu Riyama nimemkosea nini? Pamoja na kumsaidia lakini ndio amekuwa mfitini wa kazi zangu, alishanifanyia unyama huo, Shamsa Magunga katika kazi yake, leo tena karudia kwa Didas,”

“Siumii kwani sikwenda kurekodi Uingereza no, bali kwani mtu akupe sifa ambayo hauna, kama ya ukorofi na usumbufu,”anauliza Frank.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging