Google PlusRSS FeedEmail

KAJALA, WEMA SEPETU WATOANA JASHO POLISI.

                                   
Mwigizaji Kajala Masanja Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja 

Mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

Duru  zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii. 

Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake  alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema 

Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi..

Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni


Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging