Google PlusRSS FeedEmail

FEZA KESSY ATOA SOMO KWA MISS TANZANIA

MSHIRIKI wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Feza Kessy, amemtaka mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kuachia ngazi kama kweli madai dhidi yake yanamgusa nafsi yake.

“Yeye ndiye anajua ukweli, arudishe kiroho safi, tumche Mungu, katika maisha haya, hasa katika tasnia ya burudani, watu wengi sana wanadanganya, huenda alifanya hivyo bila sisi kujua nia yake, na ninaomba pia kama atafanya hivyo, watanzania tumsamehe,” alisema Feza, ambaye pia alishinda taji la Miss Dar City Center na Miss Ilala mwaka 2005.

Sitti aliyeshinda taji hilo mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ameibua mjadala mkubwa katika jamii, kufuatia madai kuwa alidanganya umri wake, kwani wakati akiwa ukumbini kujitambulisha, alidai kwamba ana umri wa miaka 18, ambao unapingwa na wadau wa kada mbalimbali.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging