Google PlusRSS FeedEmail

WASHIRIKI 3 WAONDOLEWA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER

Mchezo wa maisha halisi ndani ya jengo moja la Big Brother Africa unaendelea huku washiriki kadhaa wakiondolewa mjengoni ikiwa ni safari ya kumpata mshindi wa msimu huu uliopewa jina la ‘Hot Shots’

Jumapili iliyopita, mshiriki wa Tanzania Irene Laveda aliukwepa moto na kuwashuhudia Esther (Uganda), Sabina (Kenya) na Lilian (Nigeria) wakiondolewa katika mchezo huo.

Hadi sasa ni washiriki wa kike 8 na wa kiume 13 waliobaki katika jengo hilo huku Tanzania ikiendelea kuwakilishwa na washiriki wote wawili.

Nchi za Uganda, Zambia, Msumbiji, Kenya na Nigeria hivi sasa zinawakilishwa na mshiriki mmoja mmoja baada ya washiriki wengine kuondolewa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging