Google PlusRSS FeedEmail

JA RULE 'TEJA' AKIRI KUUZA DAWA ZA KULEVYA


Rapa Ja Rule anafahamika kwa mashairi mazito ama ya kigumu kama anavyofahamika na wapenzi wengi wa muziki wa rap ambapo ndani yake amewahi kuelezea mara kadhaa kuwa alijihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya kabla ya kupata mafanikio kupitia muziki wa Rap.

Rapa huyo hivi karibuni amekiri kuwa alikua akifanya biashara ya mnadawa ya kulevya alipokua na umri mdogo sana na akasikitika kwa kusema alikua akiwauzia wazazi wa rafiki yake ambao walikua wmeathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Ja Rule Amesema kuwa alikua akiumia kuona wazazi wa rafiki yajke ndio aliouwauzia madawa lakin akasema kwa kipindi hicho kanuni yao ilua kama wasipowauzia wao (Ja rule na timu yake) basi watauzia na watu wengine hivyo ni bora wawauzie wapate pesa ya kujikimu.

Rapa huyo alisema kabla ya kujiingiza katika Rap Maisha yalikua magumu sana na anakumbuka wakati alipohama kutoka kwa bibi yake aliekua akimlea na kurudi kwa mama yake wakati huo alipokua na umri kati ya miaka 12 au 13 ndio alijitumbukiza katika biashara hiyo na anakiri kwamba alikua akitimiza ndoto yake ya walau kupata maisha mazuri kwa kupitia biashara hiyo kutokana na hali duni ya kimaisha aliyokua nayo mama yake mzazi hata hivyo aliacha biashara hiyo mara tu baada ya mafanikio katika muziki.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging