Google PlusRSS FeedEmail

JE WAJUA VYEMA SOKO LA FILAMU NCHINI?

                Kapico Tanzania

HIVI karibuni nikiwa mtaani natembea hadi katika maduka ya kuuza filamu za Kibongo nikitaka kujua kwanini filamu za Kitanzania huuzwa kwa moja na mbili ambazo zimebatizwa kwa jina la part 1 na 2? Ikiwa ni tofauti na tasnia za filamu kwingineko.


ilikuwa ni kazi mbili zimetoka yaani filamu ya Vocha iliyosambazwa na Steps Entertainment, ikiipiku kwa mauzo filamu ya Never Give up iliyosambazwa na kampuni Proin Promotions huku kukiwa na mabadiliko ya ajabu sana sokoni kwani nilitarajia kuona sinema ya Never Give up ikikimbiza sokoni lakini haikuwa hivyo.

Soko lilikuwa nzuri kwa filamu ya Vocha, pamoja na kuwa na ubora wa washiriki katika filamu hiyo ya Never give up haikupokelewa vema, filamu hii ilikuwa na msanii nyota kutoka Ghana Van Vicker, sambamba na wasanii nyota kama Hashim Kambi, Irene Paul na wengine.

Nilipouliza wauzaji wa maduka yote walikiri kuwa sababu kubwa ya filamu hiyo kushindwa kufanya vizuri sokoni kwa sababu ya kutolewa 2in 1, jambo ambalo wauzaji hawataki kwani hawapati faida kitu ambacho si kweli kulingana nautafiti

Utafiti unaonyesha kuwa soko la filamu limeshirikiliwa na Vibanda umiza, Maktaba za kuazimisha Dvd, na sababu kubwa inayofanya hilo litokee ni sababu ya wauzaji kuwatumia wamiliki wa Maktaba kwa ajili ya kukodisha filamu hizo kwa watazamaji.

Sababu kubwa ni mtu wa Maktaba akichukua filamu yenye sehemu mbili anaikodisha kwa gharama ya 1,000/ wakati akiwa na filamu ambayo ni moja katika Dvd ataikodisha kwa gharama ya Ths. 500 tu, hilo ndio tatizo nguvu waliojijengea watu wa maktaba inalifanya soko la filamu kukosa mwelekeo.

Swali ninalojiuliza ni kwamba je wauzaji na kukodisha katika maktaba wanamsaidiaje mtayarishaji au mtu yoyote anayehusika na suala la filamu? Kama ni faida basi irudi kwa wenyewe wafaidike na biashara inayoongozwa na wamiliki wa Maktaba.

Busara ni kuangalia maslahi yanayopatikana kwa biashara ya filamu yawafikie wote na si yawe kwa upande mmoja tu, na kuaharibu mfumo wa soko la filamu baada ya watu kung’ang’ania kulazimisha Dvd ziweze kuuzwa mbili kwa sababu tu ya wamiliki wa Library ili wapete faida kwa kazi moja.

Mlaji ambaye ni mnunuzi anafirikiliwaje? Kwani kufuatia mfumo huo kumekuwa na tatizo la kulazimisha filamu kuwa ndefu bila sababu, urefushaji wa filamu hizi unamboa mtazamaji wa filamu na kuona kama ni ubabaishaji tu katika utengenezaji wa filamu hiyo.

Haiwezekani mtu asiyelipa kodi ya moja kwa moja au kukosa mikataba na wamiliki wa filamu atawale soko kwa sababu ndio mwenye uwezo wa kumwongoza msambazaji, leo sinema ikitoka kwa 1 wanagoma kununua na kulazimisha itoke sehemu mbili.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging