Google PlusRSS FeedEmail

MSHINDI WA BBA AZUNGUMZIA UJUMBE ULIOANDIKWA NA DAVIDO KWENYE MTANDAO


SIKU chache zilizopita habari zilienea kwenye mitandao ya kijamii juu ya msanii kutoka nchini Nigeria  Davido kudaiwa kuwakwaza watanzania kwa kile alichokiandika kwenye twitter juu ya watanzania kujipatia ushindi kwa njia ya kudanganya.

Hali hiyo ilitokea mara baada ya Mwakilishi kutokea Tanzania Idris Sultan kutangazwa kuwa mshindi wa Big Brother Africa Hotshots.

Mengi yamezungumzwa na watu,lakini jana mshindi wa Big Brother Africa Hotshots,Idris Sultan alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari mbalimbali miongoni mwa maswali aliyouliza ilikuwemo suala la Davido.

Ambapo mshindi huyo alisema kuwa "Kwanza ningependa kusema nahisi ilikuwa ni utani kwasababu mwishoni mwa ile sentensi kumbuka kuna alama ya utani yaani ‘Lol’ sasa nimeshangashwa kuona watu wanaanza kuhisi vibaya kuwa ni dongo kwetu hapana.Ningewataka watanzania pamoja na Davido tusiingie kwenye migogoro isiyokuwa na msingi sisi sote ni bado vijana tunatakiwa kujitangaza na kupeana support hata vizazi vinavyokuja vijifunze vitu vizuri kutoka kwetu ikiwemo Upendo na Amani kati ya Tanzania na Nigeria’Alisema Idris Sultan.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging