Google PlusRSS FeedEmail

VIPAJI VIPYA VINAIBUKA WAONGOZAJI WALE WALE- LULU

                     Elizabetn Michael
Nyota katika tasnia ya filamu  Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kudai kuwa waongozaji na watayarishaji wengi ni wale wale hakuna mpya jambo ambalo linampa hofu kuwepo kwa upendeleo kwa wasanii wapya kuliko kwa wasanii wakongwe.

“Waongozaji wa filamu ni wachache au naweza kusema kuwa ni wale wale, kila siku wasanii wanzuri wanaibuka na kuwika lakini ni vigumu hali hiyo kutokea kwa waongozaji wapya na kufanya vinzuri, tunahitaji basi watoke hata nje ya nchi kuepusha upendeleo kwa baadhi ya wasanii,”anasema Lulu.

Lulu anasema hiyo ndio moja ya sababu inayofanya wasanii wengi kutengeneza filamu zao wenyewe kama waongozaji na hata kuwa ndio watayarishaji wakuu baada ya kukosa nafasi mara kwa mara, hivi karibuni Lulu amefanikiwa kutoa filamu yake Mapenzi ya Mungu aliyomshirikisha Mama Kanumba ikiwa ni moja ya kazi zake ambazo amekuwa akiziandaa mwenyewe.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging