Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU KUUZWA BUKU JERO NI LAANA YA KANUMBA - STEVE NYERERE

            

MSANII mwenye makeke aliyekuwa mwenyekiti wa kundi la Bongo movie Unity Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ kaibukia katika uzinduzi wa kitabu cha marehemu Steven Kanumba baada ya kupotea katika tasnia ya filamu kwa muda na kutabainisha kuwa kushuka kwa tasnia ya filamu ni Laana ya marehemu Kanumba wasanii kutokuna mchango wake kimataifa.

“Hayo tunayoona wasanii kutengana soko la filamu zetu kushuka viwango ni laana ya Kanumba kwa tunayomtendea, Kanumba alipigania sanaa kimataifa na leo tunaona kazi zake pamoja amefariki lakini watu wa mataifa wanaona umhimu wa Kanumba lakini sisi tumebaki na chuki zetu,”anasema Steve.

“Nasema tena filamu zetu kuuzwa buku Jero ni laana ya Kanumba, unafiki kutopendana ni Laana ya Adam Kuambiana, tumewaacha wenzetu waliotutangulia bila chochote,”

Msanii huyo alizidi kulalamika kuwa kuna watu waliwahi kusema kuwa yeye alikuwa chanzo cha ugomvi wa marehemu na kundi la Bongo movie lakini yeye ndio kafika katika uzinduzi lakini wale waliojifanya wema hakuna hata mmoja aliyefika katika uzinduzi wa kitabu cha The Great Fallen Tree uliofanyika katika ukumbi wa Landmark Hotel.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging