
Mama yake mzazi akiongea na FC amewashukru wale wote ambao wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu na kufanikiwa kutangaza Tanzania.

“Nawashukru sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.
Kitabu hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya
Uzinduzi wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure ukiingia tu mlangoni na kazi zote za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!