
Mpenzi mmoja wa Wema kutoka Dodoma amesema kuwa anaona wazi kabisa kuwa Wema amekosa shangwe ambazo alikuwa akizipata kutokana na shamrashamra za burudani anapokuwa na Diamond katika matamasha mbalimbali.
“Mimi ni funs wa Wema leo nilipokuja katika show hii nimebaini kuwa nyota wangu kuna vitu anamiss kutoka kwa Diamond, unajua kashajizoesha hoya hoya, na anataka zifanywe na mtu wake, sasa hayupo labda ndio awatengeneze akina Mirror,”alisema shabiki huyo wa Wema alijitambulisha kwa jina la Juma Mdingo.

Wema akiwa sambamba na mpambe wake Aunty Ezekiel walikuwepo Dodoma na Morogoro kwa ajili ya show hizo ambazo zilikuwa zikitumbuizwa na Mirror Ali Luna na wasanii wengine Mirror yupo chini ya usimamizi wa Wema kupitia kampuni ya EndlessFame.
Historia inaonyesha kuwa Wema ni mtu anayependa mitoko huku akihusika sana kama vile kupanda jukwaani kucheza kuimba kidogo vitu alivyokuwa akivipata kwa Dacote lakini sasa Zari kaharibu deal!