Google PlusRSS FeedEmail

CHID BENZ AKIRI MASHTAKA YAKE LEO MAHAKAMANI
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini Bongo Fleva Rashidi Makwaro 29 maarufu kama Chid Benz leo amekiri mahakamani mashtaka matatu yanayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani y ash. 38,638, bangi y ash. 1720 na vifaa vya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikiri mashtaka hayo baada ya kusomewa upya hati yake ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Warialwande Lema.

Hakimu Lema alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mashitaka yake mahakama yake itasikiliza maelezo ya awali Februari 23 mwaka huu, kabla ya kutolewa amri hiyo Wakili wa serikali Diana Lukondo aliomba kumsoma mshtakiwa mashtaka yake upya.

Hakimu alikubali ombi hilo, Lukondo alidai kuwa Oktoba 24, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo jijini Dar es Salaam mshtakiwa alikutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 0.85.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la pili, siku na eneo la tukio la kwanza mshitakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi sivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa siku na eneo la tukio la kwanza na la pili mshtakiwa alikutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za kulevya aina ya Heroin kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Chid Benz alikiri mashtaka yote matatu, atasomewa maelezo ya awali jumatatu ijayo na dhamana yake inaendelea.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging