Google PlusRSS FeedEmail

WEMA AMTUSI SHEMEJI WA ZARI KWA KUVUJISHA PICHA AKILA UJANA NA MUME WA ZARI

                                                

Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo ambao jina lake bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya Ivan, Wema na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amemnyakua Zari, mke wa Ivan.

“Ilikuwa ni mpango wa malipizi, King na Ivan walikuwa wanaumia moyoni kumuona Diamond anatoka na Zari wakati wao wana fedha kuliko Diamond hivyo waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo Sauz wakasema watadili naye hadi kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi la kutoka naye kimapenzi au hata kupiga picha ambazo zikisambaa mitandaoni, watu watajua kwamba wamefanya malipizi,” kilisema chanzo chetu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging