Google PlusRSS FeedEmail

KAZI INAENDELEA LONDON- ESHA BUHETI

              Eshe Buheti 532

MWIGIZAJI Bora wa kike kwa mwaka 2014/2015  Esha Buheti yupo nchini Uingereza akirekodi filamu huko iliyoandaliwa na Didas Fashion ya huko inayomilikiwa na mtanzania anayeishi huko, Eshe yupo na wasanii wengine .

Wasanii walioambatana na msanii huyo ni pamoja na meneja wa kampuni hiyo kwa Bongo Husna Chobis, Yusuf Mlela wasanii hawa wanaungana na wasanii wengine kutoka nchini nyingine za Kiafrika sambamba na waingereza katika kurekodi sinema hiyo.

“Tunashukru tunaendelea vizuri katika kazi yetu iliyotuleta hapa pia tumekutana na wasanii wenzetu kuna vitu vingi tumejifunza katika tasnia ya filamu vitatusaidia sana tukirudi nyumbani,”anasema Eshe.

Mtayarishaji huyo mwenye uzoefu si mara ya kwanza kuwachukua wasanii kutoka kwenda England kwani awali aliwachukua wasanii Riyama Ali, Wastara Juma, Monalisa na Issa Mussa ‘Cloud 112’ na kutengeneza filamu ya Mateso Ughaibuni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging