Google PlusRSS FeedEmail

RAY C KIUNO BILA MFUPA KINARUDI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila 'Ray C' alijulikana kwa jina la 'Kiuno bila Mfupa' ambapo ni jina lililompa umaarufu kwa kuwa alikuwa mwembaa na uwezo wa kucheza jukwaani.

Lakini mambo yalibadilika baada ya kurejea tena kutoka kwenye tatizo la uraibu wa madawa ya kulevya na kuanza kutumia dawa ziitwazo Methadone ambazo zilimfanya anenepe kwa kiasi kikubwa kiasi cha kumfanya asiwe na kiuno chenye mfupa tena.Hata hivyo muimbaji huyo amedhamiria kurudi tena kwenye muonekano wake wa zamani kwa kufanya mazoezi makali na kutumia lishe maalum.

“20kg to go!Safari ya kupunguza mwili bado inaendelea, nashukuru nimeanza kuona mwanga mbele yangu,” ameandika Ray C kwenye picha aliyoweka Instagram inayoonesha kuwa jitihada zake zimeanza kuzaa matunda.“Si rahisi ila nimezoea kupambana na lolote mbele yangu na na uhakika ntashinda na hili pia. Am doing ths for all my fans around the world,” ameongeza.

SOURCE :  Bongo5

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging