Google PlusRSS FeedEmail

WAFANYABIASHARA HAWANA NAFASI KWANGU - WOLPER

       Jack Wolper
JAQUELINE  ‘Wolper’ amefunguka kuwa anajua thamani yake kama msanii hivyo hawezi kutumika na wafanyabiashara kwa kuwatangazia biashara zao bila kuwa na mikataba ya kueleweka au mtu kumfanyia maamuzi pasipokuwa na makubaliano na kufikia mwafaka kuhusu hilo.

“Kujenga jina katika sanaa si kazi ndogo, unapigana na kujitoa na inapotokea maarufu watu wanaanza kuona thamani ya jina ulilolijenga basi ni wakati wa kulilipia na si bure tena,”anasema.


Jack anasema hivi karibuni alikataa kupiga picha na kampuni moja baada ya kutaka apige picha akiwa ameshika bidhaa mkono wakimlaghai kuwa wamemletea zawadi pia wakitaka picha za bidhaa hiyo atumie katika akaunti yake ya kijamii, anajua walifanya hivyo kwa sababu ana watu wengi, lakini yeye alikataa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging