Google PlusRSS FeedEmail

JENNIFER LOPEZ AMUONESHEA DHARAU MARIAH CAREY

Mariah Carey ni moja ya wasanii awaliopanda juu ya jukwaa la sherehe za tuzo za chati ya billboard na kufanya onyesho la kuimba wimbo wake wa Infinity.

Licha ya umri kumtupa mkono Mariah Carey alijitahidi kuimba kadri ya uwezo wake ilikuthibitishia mashabiki wake kwamba bado yumo kwenye fani.

Wakati Mariah akiendelea kufanya yake jukwaani, kamera za mapaparazi zilitua kwa mwanamama Jennifer Lopez akichati na kuangalia picha za kwenye simu yake na kuonekana kutokujali na kufuatilia kabisa show ya mwanamuziki na mkongwe mwenzake Mariah Carey.

Kitendo hicho kimetafsiriwa kama dharau toka kwa wadau wa mastaa hao,ambao wengi kwa kutumia mitandao ya kijamii ya facebook na twita licha ya kuponda kiwango cha Mariah Carey kuwa kibovu kwenye uimbaji lakini pia walimsema Jennifer kwa kutoonyesha kujali wakati mwenzake anaimba jukwaani.

Jennifer Lopez alikaa siti za mbele pamoja na mshindi aliyetia fora kwa kunyakua tuzo nyingi usiku huo Taylor Swift ambaye alionekana mwenye hamasa na aliyefurahishwa na uimbaji wa Mariah Carey huku akimpigia makofi kila pale Mariah alipopandisha na kushusha sauti wakati wa uimbaji.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging