Google PlusRSS FeedEmail

KAJALA MASANJA AAMUA KUMPIGIA GOTO WEMA SEPETUHABARI ambazo zipo zilizothibitishwa ni juu ya msanii wa filami nchini  Kajala Masanja na miss Tanzania 2006 Wema Abraham Sepetu hawazungumzi kabisa, hali hiyo imepelekea msanii huyo kuamua kuvunja ukimya.

Kajala kaamua kuonesha jinsi gani anathamini mchango wa Wema kwenye maisha yake, na kuamua kuandika huo waraka hapo kupitia ukurasa wake wa Instagram akimuhusisha pia meneja wa Mirror Petit Man.

“Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. Najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana Mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo namboni kubwa katika kuokoa maisha yangu…

Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu.

Nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu,mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu.

Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa umma na zaidi kwa Mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu.

Nawaombea kwa Mungu muendelee na moyo huo huo kwani naamini kuna wengi bado wanawategemea ili kukomboa maisha yao kwa wakati aliyopanga mungu

Hata kitabu cha dini kilisema kuwa “huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona” najua siku moja tutaishi kama zamani.. Ahsanteni
Wapo baadhi ya mashabiki walioungana na msanii huyo kumuomba Wema Sepetu kumsamehe kwani teyari ameonesha nia ya kuomba msamaha, ingawa wapo baadhi yao waliomshambulia vikali mwanadada huyo mrembo na kudai kuwa huo ni unafki.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging