Google PlusRSS FeedEmail

KAJALA MASANJA- SWLIKALI ITAZAME WASANII KWA JICHO LA PEKEE

              Kajala Masanja

MWIGIZAJI mwenye jina kubwa Bongo movie Kajala Masanja ameingia hatua nyingine katika tasnia ya filamu pale ambapo atakuwa msanii wa kwanza kusambaza sinema zake mwenyewe baada ya kuona kuna ukiritimba katika usambazaji , jambo ambalo anaona kama linachelewesha maendeleo.

“Usambazaji ni changamoto kwa wasanii nimeliona hilo baada ya kutengeneza filamu yangu ya Pishu nimeona ni bora nifungue kampuni ya usambazaji ya Kajala Entertainment itaenda kwa wakati na kusambaza kazi zangu,”anasema Kajala.

Msanii huyo anasema kuwa kampuni yake imeajiri wafanyakazi ambao wanatakiwa kufanya kazi na kuingia sokoni sasa endapo kazi moja inachukua muda mrefu kusubiri foleni kwa msambazaji ni tatizo, hivyo anaishauri Serikali kuangalia kazi za wasanii ili waendane na kipato kulingana na umaarufu wao kwani ni vitu viwili tofauti.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging