Google PlusRSS FeedEmail

TYGA ACHANGANYWA NA PENZI LA MTOTO MDOGOPenzi la Rapa Tyga na Kylie Jenner ambaye anaumri chini ya miaka 18 linazidi kunoga huku wadau wakaribu wakitoa baraka za kutosha kwa wawili hao.

Kylie Jenner ambaye ni mdogo wake Mmwanama mwenye drama za kutosha Kim Kardashian jumapili ya mei 24 alionekana na Tyger wakila bata huku wakiangalia fainali ya mashindano ya magari ijulikana Monaco F1 Grand Prix ya mwaka 2015 ambapo Nico Rosberg aliibuka kinara wa mashindano hayo.

Mwanzo wa penzi hilo lilionekana kusakamwa na maneno ya watu kwani wengi walihoji uhalali wa Kylie Jenner ambaye anamiaka 17 iweje awe kwenye uhusiano tena wa wazi mbele ya jamii, kitendo kilichoonekana kiko nje ya maadili ya nchi ya Marekani.

Lakini siku zinavyozidi kwenda maneno hayo yanapungua na tayari shemeji wa Kylie Jenner, Dk. Kanye West ameribariki penzi hilo na kusema kwamba wawili hao wanaonekana wanapendeza kuwa pamoja hivyo wacha wandelee na penzi lao.

Tyger anaumri wa miaka 25, anaonekana mwenye furaha ndani ya penzi hilo na sasa sio siri tena kwamba wawili hao ni wapo pamoja, kwani kwa kutumia akaunti za mitandao yake ya kijamii Tyger amekuwa akipost picha zinazoonyesha akiwa na Kylie Jenner kwenye matembezi na mitoko yao ya kila siku.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging