Google PlusRSS FeedEmail

50 CENT AMPIGA VIJEMBE JAY Z

Inaonekana kutoshirikishwa kwa 50 Cent kwenye dili la Program ya Tidal mchongo unaosimamiwa na Jay Z kimemkera 50.

Wakati akifanya mahojiano na radio Real 92.3, 50 Cent alisema laiti kama angeshirikishwa kwenye idea basi Program hiyo ingekuwa bora zaidi.

“Kwanza watu wengi waliomo kwenye Program ile hawana hata hati miliki ya muziki wao. Tidal inatakiwa isambaye sehemu kubwa, sina management kwa sasa naamini ningefanya kitu kikubwa sana juu ya program ya Tidal, alisema urtis James Jackson a/k/a 50 Cent.

Program ya Tidal imeanzishwa siku kadhaa zilizopita na msimamizi mkuu ni Shawn Corey Carter a/k/a Jay Z ambapo lengo lake ni kutaka kuwasaidi wasanii wakubwa kupata fedha nyingi kutokana na kazi zao za muziki.

50 Cent alielezea tuhuma za yeye kuichukia series ya Empire inayoonyeshwa ndani ya kituo cha runinga cha Fox.

50 alisema, “Watu wanafikiri mimi naichukia Empire, hapana ukweli ni kwamba pamoja na Epire ni idea yetu iliyoibiwa lakini nawapenda washiriki wote wa series hiyo na nawaombea wafikie mbali kimaendeleo”.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging